MOSCOW,URUSI

MSHAURI  wa usalama kitaifa wa Ikulu ya White House Robert O’brien amesema madai ya kupewa sumu kwa kiongozi wa upinzani nchini Urusi Alexei Navalny yanatia wasiwasi mno na huenda yakaathiri uhusiano kati ya Marekani na Urusi.

O’brien alimtaja Navalny kama mtu jasiri mno kutokana na hatua yake ya kumpinga Rais Vladimir Putin nchini Urusi.

Ujerumani na Ufaransa walijitolea kumpa Navalny matibabu.

Kufikia sasa Wakfu mmoja wa amani ulio na makao yake mjini Berlin ulisema ndege ya kubebea wagonjwa iliyokuwa na wataalamu wa kutibu wagonjwa waliopoteza fahamu ilikuwa inajiandaa kuondoka Ujerumani kuelekea kumbeba Navalny.