LOS ANGELES,Marekani
MUIGIZAJI wa filamu ya ‘Black Panther’, ya mwaka 2018, Chadwick Boseman amefariki dunia kwa tatizo la Kansa.
Nyota huyo alijipatia umaarufu kupitia filamu amefariki akiwa na umri wa miaka 43, juzi Ijumaa.
Kifo chake kimewashtua nyota wengi ikiwa ni pamoja na Oprah Winfrey ambaye anaandika kupitia Ukurasa wake wa Twitter kuwa:Nafsi yako na ipumzike katika amani.
Filamu ya Wakada ilipata umaarufu duniani kutokana na kuigiza mila za kiafrika.Hashtag yake ilikuwa ni Wakada Forever.
Muigizaji Chadwick Boseman aliyepata umaarufu mkubwa kwenye filamu ya Black Panther kutoka studio za Marvel akiigiza kama Mfalme T’Challa amefariki dunia kwa kansa ya utumbo mpana.
Boseman mwenye umri wa miaka 43 amefariki nyumbani kwake Los Angeles akiwa na mkewe na familia yake. Taarifa zinasema aligundulika na kansa miaka minne iliyopita.