KAMPALA,UGANDA

RAIS  wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni amekosoa viongozi wa chama chake na wasomi kwa kupigania mipango ya Serikali inayolenga kupunguza mateso ya raia wa kawaida.

Museveni alisema hayo wakati akihutubia kamati kuu ya chama cha National Resistance Movement (NRM) katika Jengo la Jimbo la Entebbe.

Alisema wakati anaanza harakati za kukutana na vijana masikini wa mjini na maeneo ya makaazi duni ya Wakiso, alidharauliwa na maofisa wa NRM ambao walitaka kila kitu kiandaliwe kupitia wao.

“Vijana na watu wa kipato cha chini walipuuzwa na wasomi wa NRM. Tulipowapoteza,nilienda kuwatafuta na nilikuwa nikishambuliwa na miundo ya NRM.Walikuwa wakiniuliza kwa nini Museveni anatafuta vijana tuko hapa. Ndio maana NRM ilishinda Kampala,”alisema.

Museveni ambaye aliwataka wanachama wa chama chake kuwa mawakala wa mabadiliko,alisema masuala ya kufukuzwa kwa ardhi yanakua kwa sababu wabunge wa chama na wengine walishindwa kuhamasisha raia.