KAMPALA,UGANDA

RAIS  wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza leo kuwa siku ya kitaifa ya maombi kwa ajili ya Covid-19.

Rais huyo alisema kuwa alipata wazo hilo kutoka kwa raia wa Uganda ambaye alikuwa na maono kutoka kwa Mungu.

“Mungu alikua amemuambia katika moano kwamba ninapaswa kuanda maombi, yaandaliwe kisayansi, ili Mungu atuponye na Covid-19…Ninatangaza tarehe 29 Agosti, 2020, siku ya maombi ya kitaifa na siku ya mapumziko ya umma.Kaeni majumbani mwenu au kwenye viwanja vya nyumba zenu na muombe,” Museveni alisema katika ujumbe wake wa mtandao wa kijamii.

Hadi sasa Uganda imerekodi watu 2,679 wenye maambukizi ya virusi vya coronana vifo 28.

Serikali iliweka masharti ya kudhibiti maambukizi baada ya kuthibitisha kisa cha kwanza mwezi Machi.