LAHORE, PAKISTAN

WATU wapatao 18 wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa katika matukio yanayohusiana na mvua sehemu tofauti za mkoa wa mashariki wa Punjab nchini Pakistan hapo jana.

Maafisa wa uokoaji waliambia vyombo vya habari vya ndani kuwa nyumba kadhaa zimeharibiwa kabisa na mvua kubwa na pepo za radi katika mkoa huo na wengi wa waliokufa walipoteza maisha kutokana na tukio la kuanguka kwa paa.

“Mapaa kadhaa ya nyumba hasa za zamani zilianguka kwa sababu ya mvua katika eneo la Harbanspura la Lahore, mji mkuu wa mkoa wa Punjab, na kuwauwa watu wanne na kuwajeruhi wengine watano”, ni kulingana na maafisa wa uokoaji.

Katika tukio jingine, watu tisa wa familia moja walifukiwa chini ya kifusi wakati paa la nyumba yao liliporomoka kwa sababu ya mvua kubwa katika eneo la Mali Kalan wilayani Sheikhupura ambapo katika tukio hilo watu watatu akiwemo mtoto walifariki na wengine sita walijeruhiwa.

Sambamba na hilo, lakini katika tukio jengine mama na watoto wake wanne walipoteza maisha wakati paa la nyumba yao lilipoanguka katika mkoa wa Mandi Bahauddin.

Aidha taarifa ziliongeza kuwa wafanyakazi wapatao watatu walifukiwa baada ya maporomoko ya ardhi yalitokea kwenye mgodi wa makaa ya mawe ambapo walikuwa wakifanya kazi katika eneo la Qasba Bhal wilaya ya Chakwal.

Wafanyikazi wengine watano pia waliendeleza majeraha katika tukio hilo la bahati mbaya.

Mapema wiki hii, Idara ya Hali ya Hewa ya Pakistan ilionywa kunyesha kwa mvua kubwa kuanzia siku ya Jumatano na kuendela kwa siku tatu hadi nne.

Mvua kubwa inayoendelea kunyesha imesababisha mito ya Punjab na mkoa wa kaskazini magharibi wa Khyber Pakhtunkhwa kufurika na hivyo kusababisha maafa makubwa kwenye majimbo hayo.