NA FATMA AYOUB, MCC

NAHODHA wa timu ya mpira wa Nage ya Ndijani Mtawanga Mwanaisha Idrisa Khatibu ,amesema wapo katika mazoezi makali ili kuhakikisha wanafanya vyema katika michuano inayokuja hivi karibuni.

Aliyasema hayo baada ya kufunguliwa kwa mchezo huo ambao utashirikisha timu za Mkoa wa Kusini Unguja.

Alisema tayari wameanza kujipanga na wanaamini kuwa watashinda katika mashindano hayo.

Alifahamisha mwaka jana walishiriki mashindano hayo kiwilaya na wakaibuka kuwa washindi.

Alifahamisha kuwa Nage ni mchezo kama ilivyo michezo mingine hivyo anawashauri wanawake wa Mkoa wa Kusini Unguja kujitokeza kwa wingi kushiriki mchezo huo.

MALEZI ya pamoja katika miaka ya nyuma ni njia moja wapo iliyosaidia jamii kupambana na majanga mbali mbali yanayowasibu watoto hasa kwa wakati huu tulionao.

Malezi hayo yalisaidia kwa hali moja ama nyengine kutatua shida nyingi za kijamii, ikiwemo hata mlo wa siku baina ya familia moja na nyingine.    

Wazee wa zamani walikuwa na ushirikiano wa dhati katika malezi ya pamoja kwa watoto, ili watoto wakue kwenye misingi bora na ya historia tena yenye heshima.

Ndio maana leo naweza kusema kuwa malezi ya pamoja kama yakirejeshwa yanaweza kuwa mwafaka kumaliza matatizo kadhaa hususan suala la udhalilishaji kwa wanawake na watoto.

Kutokana na hali hiyo watoto walikuwa na tabia njema kwa ndugu, jamaa na marafiki na watu wengine kwa ujumla.

Leo tunashuhudia mporomoko mkubwa wa maadili kwa watoto wadogo, vijana n ahata wazee jambo ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa kuweka kwa vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia katika familia na jamii.

Kwa mukhtaza huo basi tunapaswa kujiuliza kwanini tusiwe tayari kuyarejesha malezi ya pamoja?, ule utamaduni tuliozuzowea kutoka kwa mababu na mabibi zetu uko wapi? Huu ni utandawazi au utandawizi uliotuibia utamaduni wetu wa kale.

Mababu na mabibi zetu zamani hawakushuhudia vitendo vya ubakaji, ulawiti na ukatili mwengine na kama vilikuwa vikifanyika basi ni kwa siri mno, lakini leo hii ni nadra kwa siku kutosikia kwenye vyombo vya habari.

Jamii sasa imezungukwa na majanga mbali mbali likiwemo janga zito la udhalilishaji kwa wanawake na watoto,hii inatokana na sababu kadhaa, lakini sababu ya msingi ni kuondoka kwa malezi ya pamoja.