NA ZAINAB ATUPAE

NUSU fainali ya kwanza ya mashindano ya Bwejuu Super Ndondo Cup inatarajia kupigwa leo.

Akizungumza na gazeti hili mratibu wa mashindano hayo Najim Suleiman, alisema mchezo huo utawakutanisha Bwejuu Mjini na Ushikaji Mgumu.

Alisema mechi hiyo itakuwa ya ushindani mkubwa, hivyo aliwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi kuangalia mpambano huo.

Alisema nusu fainali ya pili inatachezwa kati ya Tupogo na Kazi kazi.

Timu ya Bwejuu Mjini imeingia hatua hiyo ikiwa na pointi saba, huku Ushikaji Mgumu akiwa na pointi saba pia.

Tumu ya Tupogo imeingia ikiwa na poniti tano na Kazi Kazi ikiwa na pointi nne ambapo michezo hiyo itapigwa majira ya saa 10:00 uwanja wa BZL.