TOKYO, Japan
MCHEZAJI nyota wa tenisi raia wa Japan ambaye pia ni mshindi mara mbili wa mashindano ya ‘Grand Slam’ Naomi Osaka, amejitoa kwenye robo fainali ya mashindano ya wazi ya duniani yanayofanyika New York, Marekani.
Hatua hiyo ikiwa ni kupinga kitendo cha polisi kumpiga risasi Mmarekani mweusi, Jacob Blake ambaye hakuwa na silaha huko Wisconsin.
Osaka ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa ‘twitter’, hatarajii kitu kikubwa kutokea kwa kujitoa kwake kwenye mashindano hayo, lakini, kama akiweza kuanzisha mjadala katika mchezo huo unaomilikiwa zaidi na wachezaji weupe.
“Naona hiyo ni hatua katika muelekeo sahihi”, aliandika Osaka.(AFP).