WAPENZI wasomaji wetu wa Zanzibarleo tkatika safu yetu hii ya maakuli nimewatayarishia upishi wa Dhokra ambao ni adimu hapa kwetu.
Hata hivyo, baadhi ya siku familia inaweza kupika ikiwa ni kubadilisha mapishi, ili kuweza kuupika upishi huu ni lazima kuwa na mahitaji haya yafuatayo:-
VIPIMO
Unga wa mahindi au wa mchele – ¼ magi
Unga wa dengu – 2 magi
Mtindi (yogurt) – 1 kopo
Manjano – 1 kijiko cha supu
Kitunguu saumu (thomu/galic) – 2 vijiko vya supu
Pilipili ya chupa ya Sambal – 2 vijiko vya supu
Chumvi – 1 kijiko cha supu
Sukari – 6 vijiko vya supu
Pilipili mbichi – upendavyo
Kotmiri – kiasi
Baking powder – 1 kijiko cha chai
Ndimu – 1
Rai – 2 kijiko cha supu
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
- Changanya yogurt, unga wa mahindi na unga wa dengu vizuri
- Kata vitunguu, kotmiri, na pilipili mbichi vipande vidogo.
- Kisha uchanganye na vipimo vilivobaki isipokuwa baking powder
- Paka kisinia kidogo mafuta tia mchanganyiko kwenye bakuli kiasi
- Tia baking powder changanya kisha tia kwenye kisinia uliyoitayarisha.
- Chukuwa sufuria kubwa kidogo tia maji kikombe kimoja kisha weka bakuli jengine ndani ya sufuria ya maji.
- Tia kisinia cha mchanganyiko juu ya kibakuli funika vizuri upike kwa mvuke (steam) muda wa saa hivi.
- Weka mafuta Kijiko kimoja cha chai kwenye kisufuria kidogo ukaange rai kotmiri na pilipili mbichi.
- Ikishaiva dhokra utanyunyiza kwa juu pamoja na masala ya unga
- Kidokezo
- Unaweza kuweka kwenye friji ukafanya kidogo kidogo