PARIS, Ufaransa
KOCHA wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps, amesema, kiungo mahiri wa Manchester United, Paul Pogba, amekutwa na virusi vya ‘corona’, na kwamba mchezaji huyo kwa sasa amejitenga kwa siku 14.
Hatua hiyo inamfanya Pogba kukosa mechi ya Ufaransa katika Ligi ya Mataifa ya UEFA dhidi ya Sweden itakayochezwa Septemba 5 ugenini na mechi nyengine dhidi ya Croatia itakayochezwa jijini Paris siku tatu baadaye.
Hata hivyo, Pogba atakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuichezeka klabu yake ya Manchester United watakapofungua rasmi kampeni zao za Ligi Kuu ya England (EPL) msimu huu wa 2020-21 dhidi ya Crystal Palace.
Mechi hiyo itachezewa uwanja wa Old Trafford Septemba 19.(AFP).