NEW YORK,Marekani
MOJA ya taarifa iliyopo katika Mtandao wa ‘TMZ’ ni kumhusu Wakili wa R. Kelly, ambapo ameomba mteja wake achiliwe huru mara moja baada ya kusemekana kwamba ameshambuliwa na mfungwa mwenzake.
Steve Greenberg amesema mteja wake alishambuliwa katika kituo cha kurekebisha tabia cha Chicago, ambapo Kelly anasubiri kusikilizwa kwa kesi yake dhidi ya madai ya unyanyasaji wa kingono.
Kiwango cha majeraha bado hakijafahamika, Bwana Greenberg amesema kupitia mtandao wa Twitter.
Kelly hajapatikana na hatia kwa makosa kadhaa ikiwemo ya unyanyasaji dhidi ya watoto na biashara ya ngono.
Taarifa za madai ya kushambuliwa kwake kuliripotiwa kwa mara ya kwanza na tovuti ya habari ya TMZ, ambayo imesema kwamba mfungwa mwenzake alianza kumpiga Kelly ngumi akiwa amekaa kwenye kitanda chake.