SKOPJE, NORTH MACEDONIA
RAIS Stevo Pendarovski wa North Macedonia, ameagiza kuundwa kwa serikali mpya itakayomshirikisha kiongozi mkuu wa muungano wa upinzani, Zoran Zaev.
Shirika la Habari la Media (MIA) limeripoti muungano wa “Tunaweza” ukiongozwa na kiongozi wa Zaev na Besa Movement Bilal Kasami ulishinda kwa asilimia 35.89 ya kura na viti 46 vya bunge katika uchaguzi wa mapema wa bunge uliofanyika Julai 15.
“Kwa kuzingatia Ibara ya 84, kwa mujibu wa Kifungu cha 90 cha Katiba na pendekezo la muungano wa ‘Tunaweza’, namtaja Zoran Zaev, kiongozi wa SDSM na mbunge, kuwa waziri mkuu wa kuteua serikali,” Pendarovski alisema katika hafla iliyofanyika hapo jana.
Aliongeza kuwa Zaev atakuwa kwenye serikali mpya na anaamini atafuata “njia sahihi” kuelekea Jumuiya ya Ulaya (EU) na kujenga wazo la “jamii moja kwa wote” lililowekwa huru kutoka kwa utaifa na ubaguzi wa kikabila.
Nae kiongozi wa SDSM alisema anaamini kuwa nchi hiyo itajipatia maendeleo makubwa hasa katika jumuiya ya Ulaya sambamba na ustawi na utulivu wa muda mrefu, maendeleo ya uchumi, mapambano dhidi ya uhalifu, rushwa na kusafisha mahakama.
Kufikia sasa, mazungumzo kati ya vyama vya siasa hayajatoa matokeo ya kuunda angalau viti 61 kati ya jumla ya viti 120 katika Mkutano wa Makedonia ya Kaskazini.
Zaev alisema kwamba ataanza tena mazungumzo na Ali Ahmeti, kiongozi wa Jumuiya ya Kidemokrasia ya Ushirikiano, ambayo imeshinda viti 15 bungeni.