KIGALI,RWANDA

KITUO cha Rwanda Biomedical Center (RBC) kimeelezea uamuzi wake wa kuwaruhusu waliowasili nchini kuwasilisha vipimo hasi vya Covid-19 vilivyofanywa ndani ya siku tano kabla ya kuondoka walikotoka.

Tangu kufunguliwa nchi hiyo kwa wasafiri wa kimataifa mwanzoni mwa Agosti,mahitaji ya usafiri yaliongezeka.

Mkurugenzi Mkuu wa RBC Dk Sabin Nsanzimana,alitangaza mabadiliko yaliyofanywa kwa sababu ni vigumu kwa wasafiri wengi kupata matokeo kutoka katika na kufika kwa siku tatu.

Mabadiliko hayo ni ya lazima kwa wasafiri wanapoingia Rwanda tokea  kuanzia Agosti 15.

RBC ilisisitiza kwamba matokeo ya pekee yanayokubaliwa ni SARS-CoV 2  inayoonesha muda halisi wa vipimo pamoja na vipimo vyengine ambapo vipimo vya haraka havitokubaliwa.

Pia wasafiri wote wanaofika lazima wajaze fomu ya abiria na awe na cheti cha matokeo ya COVID-19 kwenye wavuti ya RBC kabla ya kuwasili.

Wasafiri wote wanaofika Rwanda watapimwa kwenye kiingilio na kupimwa kwa mara ya pili ili kuthibitisha matokeo hasi ya vipimo yaliyofanywa kabla ya kuwasili.

Wasafiri pia watatakiwa kusubiri masaa 24 kwa ajili  ya matokeo ya vipimo vyao katika hoteli ya iliyoteuliwa na wanapokuwa katika kipindi cha kusubiri,wanapaswa kufuata hatua zote za kuzuia maambukizi zilizotangazwa na Wizara ya Afya.

Serikali ya Rwanda ilijadili viwango maalum katika hoteli maalumu za usafirishaji kwa kipindi cha masaa 24 cha kusubiri.

Baada ya kupokea matokeo hasi ya vipimo,wasafiri wataruhusiwa kutoka nje ya hoteli,na ikiwa matokeo ni mazuri,wasafiri watatibiwa hadi watakapopona, kwa gharama yao wenyewe.

“Tunawahimiza wasafiri wote kuwa na bima ya kusafiri ya kimataifa,” taarifa kutoka RBC ilisema.