NA HANIFA SALIM

WATENDAJI wa serikali wametakiwa kuwa mstari wa mbele kuyatangaza mafanikio na maendeleo yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 10 ya uongozi wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein.

Wito huo ulitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Hemed Suleiman Abdalla, wakati akizungumza na watendaji wa Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Mkoani, katika ukumbi wa mikutano wilayani humo.

Alisema kutokana na juhudi zilizofanywa na serikali za  kuwaletea wananchi maendeleo, ni vyema mafanikio hayo kuzitangazwa.

“Ziara hii ya leo nazungumzia kipindi hiki cha miezi miwili iliyobakia kabla ya uchaguzi, watendaji wale ambao mna mamlaka ya kutunza mali za serikali, muzitunze kwa nguvu zote na kufuata sheria, kwani hatutakubali mtu yeyote kuvunja taratibu,” alisema.