NA NASRA MANZI

MKUU wa Mkoa wa Mjini Magaharibi, Hassan Khatib Hassan, amewataka viongozi wa madhehebu mbali mbali ya kidini  kuendelea na maombezi ya kuiombea dua nchi kuelekea uchaguzi Mkuu ujao.

Akifungua kongamano la amani Zanzibar kwa wadau wa mradi wa Amani wa dini mbali mbali lilolofanyika katika uwanja wa Maisara Suleimani, alisema ni vyema kushirikiana kwa pamoja bila ya kuonesha ubaguzi katika kusimamia amani  ili uchaguzi utakapomalizika wananchi kuendelea na shughuli zao za kimaendeleo.

Pia alisema kwa siku ambazo zilizobakia umuhimu wa amani kuendelezwa, lakini kwa atakaejitokeza kuchafua amani  iliyopo ni lazima kuchukuliwa hatua za kisheria.

“Serikali tutasimamia kwa gharama yeyote suala la amani  na wananchi kuendelea na shughuli zao, lakini atakaekwenda kinyume na hili hatua za kisheria zitafuata” alisema.