ASUNCION, Paraguay
NYOTA wa zamani wa Brazil, Ronaldinho Gaucho, ametoka kizuizini alipokuwa anashikiliwa kwa zaidi ya miezi mitano baada ya mahakama moja nchini Paraguay kumuhukumu adhabu hiyo kutokana na madai ya hati bandia ya kusafiria.

Gaucho ambaye ni mshindi mara mbili wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia ya ‘Ballon d’Or’, ni mmoja ya wachezaji waliofanya makubwa katika soka la dunia, akitwaa tuzo mbalimbali ikiwemo Kombe la Dunia mwaka 2002 akiwa mchezaji kinda nyakati hizo
Kiungo huyo wa zamani wa klabu za PSG, Barcelona na AC Milan, alikuwa anashikiliwa na mamlaka za usalama za Paraguay pamoja na kaka yake, Roberto de Asas ambaye anatambulika kama meneja wa nyota huyu wa zamani .

Nje ya soka Gaucho anatajwa kama mchezaji anayependa anasa na maisha ya ufahari yaliyochangia kutofanikiwa zaidi katika soka na hata sakata hill la kuingia Paraguay kwa hati ya bandia inaelezwa walikuwa wanakwenda katika uzinduzi wa moja ya kumbi za starehe ya usiku maarufu kama Cassino.(Goal).