LEGENDI Ronaldo  nyota wa zamani wa Timu ya Taifa ya Brazil na klabu ya Barcelona, amesema kuwa timu yake ya zamani itafanya makosa ikiwa itamuuza mchezaji Lionel Messi.

Messi mwenye miaka 33 amekuwa kwenye hesabu za kuondoka ndani ya Barcelona, baada ya timu yake kupokea kichapo cha mabao 8-2 mbele ya Bayern Munich kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ronaldo anaamini kwamba Barcelona ina nafasi ya kufanya vizuri kwa wakati ujao, ila inaweza kuyumba kidogo ikiwa itamruhusu Messi aondoke ndani ya kikosi hicho.

Kipigo hicho cha udhalilishaji kilimfanya Messi amshushie lawama rais wa timu hiyo Josep Bartomeu, kwa kudai kuwa ana maamuzi mabovu yanayoiyumbisha timu hiyo.

Ronaldo alicheza ndani ya Barcelona mwaka 1996-97 bado anaamni kuwa Messi anahitajika ndani ya Barcelona.

 ‘Messi ni mchezaji muhimu ndani ya Barcelona kwa sasa kama ningekuwa ndani ya Barcelona nisingemuacha aondoke kwa kesi yoyote ile ambayo ingetokea.