KATIKA safu yetu ya mapishi leo hii nimewatayarishia pishi mwanana la Rosti la nyanya chungu na dagaa kavu.

MAHITAJI

Dagaa
Tungule
Kitunguu maji
Ndimu au limao
Nyanya chungu /ngogwe
Chumvi
Mafuta,Nazi

JINSI YA KUANDAA

1 Andaa dagaa wako kisha waoshe vizuri tia chumvi na ndimu waache pembeni

2: Andaa tungule, kitunguu na nyanya chungu weka pembeni pia.

3: Chukua sufuria tia jikoni weka mafuta yakipata moto tia dagaa na kaanga kiasi weka na vitunguu na endelelea kukaanga hadi viwe na rangi nzuri.

4: Weka nyanya chungu na kaanga tena kwa muda kisha malizia tungule na kaanga hadi nyanya ziive,kisha tia maji kidogo na ndimu tena, na chumvi.

Malizia kwa kuttia tui lako halafu wacha vichemke kwa dakika 3 kisha toa na dagaa zako zitakuwa tayari kuliwa.

5: Unaweza kutumia dagaa aina yoyote ile ila lazima wawe wa kavu.