KIGALI,RWANDA
BAADA ya kuruhusiwa tena kwa wasafiri wa kigeni kutokana na janga la Covid-19, Rwanda inakabiliwa na changamoto ya vipimo vya wageni hao vilivyofanywa kwa njia ambayo Wizara haikuridhika nayo.
Kutokana na hali hiyo Maofisa wa usafiri wa ndege walilazimika kuwatenga abiria hao wa kigeni mpaka vitakapofanyika vipimo na kutoa matokeo mapya ya virusi vya corona.
“Baada ya kufungua uwanja wa ndege wa nchi hiyo, tumepokea abiria wengine ambao walikuja na majibu ya vipimo vya Covid-19 ambavyo upimaji wake hatujauukubali,” alisema Dk. Daniel Ngamije .
Waziri wa Afya wa Rwanda Dk. Daniel Ngamije alisema hatua hiyo inawapa mzigo wa ziada Maofisa wa nchi hiyo kwani hulazimika kuwatenga na kuwapima ili kujua afya zao.
Ngamije alisema hayo wakati akizungumza na Mkurugenzi wa Mkoa wa OFisi ya Shirika la afya Duniani kwa Afrika Dk Matshidiso Moeti, pamoja na waandishi wa habari juu ya maswala yanayohusiana na janga hilo.
Rwanda iliruhusu tena usafiri wa ndege Agosti 1,mwaka huu ambapo iliruhusu ndege za biashara ili kuendelea kufanya kazi ndani nan je ya nchi baada ya zaidi ya miezi minne ya kusimamishwa kwa sababu ya janga la Covid-19.
Pia alisema wasafiri wote wanaofika Rwanda watapimwa mara mbili kabla ya safari ili kuthibitisha kama hakuna mwenye maambukizi.
Rwanda inatumia vipimo vya PCR katika kuthibitisha vipimo vyake vya Covid-19.
Dk Menelas Nkeshimana alisema vipimo vya PCR ndivyo vinavyotakiwa kuliko vipimo vyengine vya Covid-19.
Waziri wa afya Dk Ngamije pia alitaja changamoto zaidi ambazo Rwanda inakabiliwa katika mapambano yao dhidi ya virusi, ambapo alionyesha tishio la usafiri wa kutumia njia za mipakani katika mkoa huo.