NAIROBI, KENYA
SKULI za binafsi nchini Kenya ziko hatarini kutolewa katika dhamana ya mikopo na Serikali kufuatia mipango ya Wizara ya Elimu ya kuzifunga kutokana na athari za Covid-19.
Hatua hiyo inatokana na wasiwasi kwamba skuli nyingi za kibinafsi zinaweza kufunga kabisa huduma zake kwa sababu ya corona.
Katibu wa Baraza la Mawaziri la elimu George Magoha alisema kwamba ufunguzi wa taasisi za ufundishaji utadhaminiwa kutokana na mwenendo wa Covid-19,hata kama Wizara ina mipango ya kutoa mkopo wa Shilingi bilioni saba kwa skuli za binafsi.
Alisema Serikali iliwataka watoto kukaa nyumbani, kwani ilibainika kuwa wanafunzi wanaweza kuwa ndio waenezaji wakubwa wa Covid-19 endapo skuli zitafunguliwa tena kabla ya janga hilo kudhibitiwa nchini.
“Ni salama kwa watoto wetu kuwa nyumbani, kwa kipindi hichi cha janga tulilonalo,”alisema.
Alisema Kenya ilifunga skuli ili kulinda watoto wa Kenya kwa sababu kila mtoto ana haki ya kuishi.
Prof Magoha alisema kufungwa kwa skuli kulitokana na mwongozo wa Wizara ya Afya juu ya mwenendo wa maambukizi ya Covid-19 na mashauriano na wadau wa elimu.
Baadhi ya skuli za kibinafsi zilifungwa kwa muda mrefu na baada ya wazazi kukataa kulipa ada ya skuli,Prof Magoha alisema Wizara ya Elimu itatoa mikopo kwa wamiliki wa skuli binafsi wanaostahili pekee.
Alisema mikopo hiyo inatolewa ili kuokoa taasisi ambazo zinakaribia kufilisika moja kwa moja na kuwataka wazazi wenye watoto katika skuli binafsi kujitahidi kulipa sehemu ya ada ya skuli ili kuzifanya ziendelee.