BEIRUT,LEBANON

WAZIRI mkuu wa Lebanon Hassan Diab ametangaza kujiuzulu kufuatia mripuko wa wiki iliyopita mjini Beirut.

Kwenye taarifa yake kupitia televisheni,Waziri mkuu Diab alisema anachukua hatua hiyo ili aungane na watu wa Lebanon na kwa pamoja wapiganie mabadiliko.

Rais Michel Aoun alikubaliana na hatua hiyo ya Serikali kujiuzulu.

Alisema wanasiasa wanatakiwa kuona aibu kwa sababu ufisadi ndio umesababisha janga hilo lililofichwa kwa miaka saba.

Baadhi ya mawaziri tayari walikuwa wamejiuzulu hapo kabla kufuatia maandamano makubwa ya kuipinga Serikali kuibuka baada ya mripuko huo kutokea.