KAMPALA, UGANDA

WIZARA ya Mambo ya nje nchini Uganda imefungua mipaka kwa Waganda waliokaa kwenye nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ili warudi nyumbani.

Huduma hiyo inatokana na kurudishwa Waganda waliokwama nje ya nchi kutokana na athari za janga la Covid-19.

Serikali ilisema ilikuwa katika mipango ya kutafuta njia ya  kuwarudisha Waganda kwa njia ya usalama.

Hapo awali, malori tu ya kubeba mizigo ndio yaliyoruhusiwa kuingia nchini baada ya kuzuka kwa Covid-19 mnamo Machi.

Waziri wa Mambo ya nje wa Nchi, Okello Oryem, aliiambia Daily Monitor katika mahojiano ya simu kwamba Waganda wanapaswa, kupata kibali kutoka kwa Tume Kuu ya Uganda katika nchi hizo na kuwasilisha cheti cha Covid-19 kabla ya kuingia Uganda.

“Waganda, ambao wanataka kurudi kwa barabara kutoka EAC wanapaswa kuwa na cheti cha Covid-9 sio zaidi ya wiki na lazima wapate idhini kutoka kwa balozi zetu. Wanapofikia mipakani wanastahili kupimwa mara nyengine kabla ya kusafirishwa,” Oryem alisema.