LONDON, England

BOSI wa Manchester United  Ole Gunnar Solskjaer amesema  mshambuliaji Anthony Martial hivi sasa yupo katika kiwango bora.

Mfaransa huyo anayevaa jezi nambri 9 ameanza vibaya  mwanzoni mwa msimu, lakini ameimarika na kuongeza imani kwa Solskjaer katika uwezo wake wa kucheza safu ya ushambuliaji  na kufunga mabao 23 msimu huu.

Mazoezi  yamemsaidia sana na kumpa faida ya kumfanya kuwa mchezaji wa ‘nguvu zaidi’ na kumweka katika hali nzuri ya kazi yake.

‘Napenda jinsi ya ufungaji wake wa mabao,’alisema  Solskjaer.‘ Najua anaweza kufanya makubwa ulimwenguni. yuko kwenye mazoezi na anafanya kazi kwa nguvu zake.

‘Yeye yuko katika kiwango bora cha kazi yake. Kuna zaidi yanakuja kutoka kwa Anthony’.