ALGIERS, Algeria
KLABU ya Tottenham Hotspurs imeingia kwenye mbio za kumfukuzia nyota wa Brentford raia wa Algeria, Said Benrahma.

Benrahma anayetajwa kama ‘Messi wa Algeria, amekuwa na kiwango bora msimu huu na hivyo, kumvutia meneja wa Spurs, Jose Mourinho, ambaye anataka kukisuka kikosi hicho.
Benrahma alifanikiwa kufunga mabao 17 na kutengeneza pasi 10 kwa kikosi cha Thomas Frank katika msimu ambao karibu uliwaona wakishinda nafasi ya kupanda Ligi Kuu ya England.

Miamba hiyo ilipoteza mechi dhidi ya Fulham katika mchezo wa mtoano wa fainali.
Chelsea na Arsenal hapo awali zilihusishwa na uhamisho kwa winga huyo sawa na Leeds United na Crystal Palace.

Benrahma anatarajiwa kugharimu kiasi cha pauni Milioni 25, ada ambayo inaweza kuonekana kuwa ya thamani huku Tottenham wakijipanga kuimarisha safu ya ushambuliaji.(Goal).