ZASPOTI
KLABU ya Stoke City wamesaini kiungo wa zamani wa Chelsea, John Mikel Obi.
Nahodha huyo wa zamani wa Nigeria mwenye umri wa miaka 33, alikuwa mchezaji huru baada ya klabu ya Trabzonspor ya Uturuki kwa makubaliano ya pande mbili.
Mikel alicheza mechi 249 za Ligi Kuu ya England akiwa na Chelsea kwenye kipindi miaka 11 akiitumikia klabu hiyo Stamford Bridge kabla ya kuondoka mwaka 2017.


Ameshinda mataji ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Ligi ya Europa, Ligi Kuu, Kombe la FA na Kombe la Ligi akikipiga na miamba hiyo ya jijini London.
Baada ya kuondoka Chelsea alijiunga na miamba ya China ya Tianjin TEDA na alitupia kipindi kifupi kukipiga na Middlesbrough mwaka 2019.


Bosi wa Stoke, Michael O’Neill alisema: “Nilivutiwa naye wakati tulipokutana kwa mara ya kwanza na alielezea kile anachotaka kutoka kwa awamu inayofuata ya kazi yake.
“Tulitumia masaa manne kuzungumza na aliweka wazi anataka kurudi kwenye Ligi Kuu ya England na kumaliza kazi yake huko na tunatarajia anaweza kufanya hivyo na Stoke City.”


Mikel alishinda mechi 89 za Nigeria, akicheza katika fainali mbili za Kombe la Dunia na kusaidia Super Eagles kushinda Kombe la Mataifa ya Afrika 2013, kabla ya kutangaza kustaafu kwake kimataifa majira ya joto msimu uliopita.


Klabu ya daraja la kwanza ya Stoke alishinda michezo yao minne iliyopita mnamo 2019-20 kuondoka na hatari ya kuteremka daraja na kumaliza nafasi ya 15 chini ya bosi wa zamani wa Ireland ya Kaskazini, O’Neill.(Goal).