DAMESKI,SYRIA

MWAKILISHI  wa kudumu wa Uturuki katika Umoja wa Mataifa amekosoa vikali kimya cha umoja huo kuhusiana na ukiukaji wa mamlaka ya kitaifa ya kujitawala ya Syria unaofanywa na Marekani na Uturuki.

Bashar al-Jaafari alitoa lawama hizo katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kilichofanyika kwa njia ya mawasiliano ya video wakati alipoashiria kuwepo kijeshi kinyume cha sheria askari wa Marekani na Uturuki.

Umoja wa Mataifa na baraza lake la usalama, zilipuuza mashitaka yaliyowasilishwa mbele yake mara kadhaa na Damascus dhidi ya uvamizi wa Marekani na Uturuki.

Mbali na kuukosoa Umoja wa Mataifa kutokana na kunyamazia kimya madola vamizi ya Marekani na Uturuki yanayokalia kwa mabavu maeneo ya Syria, Al-Jaafari aliutaka umoja huo na baraza lake la usalama zivunje kimya chao hicho na kuchukua misimamo madhubuti kuhusiana na suala hilo.

Hivi sasa Marekani na Uturuki zilijiingiza kijeshi huko Syria kinyume cha sheria na bila ya kibali cha Serikali ya nchi hiyo kwa kisingizio cha kupambana na makundi ya kigaidi.

Majeshi ya Marekani na Uturuki yalipiga kambi Syria kwa kisingizio hicho cha kupambana na ugaidi licha ya kuwa nchi hizo mbili ni miongoni mwa waungaji mkono wakuu wa magenge ya kigaidi yaliyoko nchini humo.

Mgogoro wa Syria ulianza mwaka 2011 kwa hujuma na mashambulio makali ya makundi ya kigaidi yanayoungwa mkono na Uturuki, Saudi Arabia, Marekani na waitifaki wao kwa lengo la kubadilisha mlingano wa nguvu za kijeshi katika eneo la Asia Magharibi kwa manufaa ya utawala wa Israel.