NA JOSEPH NGILISHO, ARUSHA

TAASISI ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa Mkoani Arusha {TAKUKURU} imefanikiwa kuokoa shilingi milioni 195.6 za wajasiliamali waliokuwa wamedhulumiwa na wamiliki wa kiwanda cha Kijenge Animal Productcha cha Jijini Arusha.

Kaimu Kamanda wa TAKUKURU Mkoani Arusha,James Ruge alisema hayo jana ofisini kwake na kueleza kuwa kiasi hicho ni sehemu tu ya shilingi milioni 289 za wajasilimali sita wa Arusha. 

Ruge alisema kuwa fedha hizo zilikuwa ni za mauzo ya wajasiliamali hao yaliyopokelewa na kiwanda hicho Januari mwaka huu na TAKUKURU Arusha, inaendelea na uchunguzi wa kiasi kilichosalia cha shilingi milioni 99 zinalipwa na watuhumiwa ndani ya mwezi mmoja. 

Alisema wajasiliamali waliotaka kudhurumiwa na kiasi kwenye mabano walicholipwa ni pamoja na Michael Mtana {Tsh 50,725,450}, Issa Mushi {Tsh 53,258,00}, Keneth Lauwo{Tsh 19,639,200}, Gregory Mukabi { Tsh 24,125,760}, Leo Marandu {Tsh 28,793,040} na Ahmed Mavura {Tsh 13,622,400}.

Kamanda huyo alisema kuwa TAKUKURU Mkoani Arusha, ilipokea taarifa Julai 8, mwaka huu kutoka kwa wajasiliamali hao sita wakieleza kuwa waliuza mazao {NAFAKA} kwa kampuni ya Kijenge Animal Products iliyopo Jijini Arusha kwa nyakati tofauti tangu Januari mwaka huu, lakini hawakuweza kulipwa fedha zao za kiasi cha shilingi milioni 289. 

Ruge aliendelea kusema kuwa katika kufuatilia bila ya mafanikio walikwenda kwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha mei 28 mwaka hu una Mkuu wa wilaya aliwaita wamiliki wa kampuni ya Kijenge Animal Products kujibu tuhuma na kampuni hiyo ilimtuma mwanasheria wake Mike Honest .