NA HADIJA WAZIRI, MAFIA

TAMASHA la vyakula vya asili kisiwani Mafia limefunguliwa jana na litafanyika kwa muda wa siku tatu mfufulizo.

Tamasha hilo linafanyika katika kiwanja cha Mkunguni Mjini Kilindoni na limewashirikisha wachezaji ngoma za asili, mbio za Marathon, Mashindano ya Ngarawa na Baiskeli ambapo  washindi  wameandaliwa zawadi mbali mbali. 

Akifungua tamasha hilo ofisa Utamaduni Wilaya Mafia Juma Magomba, amewataka wananchi wa Mafia walijitokeza kuonyesha vipaji vyao na kushirikiana kutangaza asili ya kisiwa cha Mafia.

Nae ofisa michezo kisiwa cha Mafia Mwinsani Ngomo amewataka wazazi kutowaficha watoto walemavu na badala yake wawatoe ili kushirikiana na watoto wenzao katika kukuza vipaji vyao.   

Aidha alisema tamasha hilo ni kwa ajili ya wananchi wote wa Mafia hivyo wote wanakaribishwa kuona vivutio mbali mbali vilivyopo Mafia.