NA TIMA SALEHE, DAR ES SALAAM

KAMATI ya nidhamu ya Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) imemfungia aliyekuwa kocha mkuu wa klabu ya Yanga Luc Eymael kutojihusisha na soka nchini kwa miezi 24.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya kocha huyo kudaiwa kutoa maneno machafu kwa klabu ya Yanga na Shirikisho wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar mkoani Morogoro..

 Akizungumza na waandishi wa habari mjumbe wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, Alex Mushumbusi, alisema kamati ya nidhamu imempa adhambu kutokana na makosa mawili.

Kosa la kwanza nikutoa kauli chafu kwa klabu ya Yanga ambapo atalipa faini ya Shilingi Milioni 5 na kutojihusisha na soka kwa muda wa miezi 24.

 Aidha alisema kosa la pili la kocha Luc ni kutoa kauli chafu kwa TFF na kulituhumu kuwapendelea Simba, hivyo atatakiwa kulipa faini ya shilingi milioni 5.

 Alisema kufuatia adhabu hizo walimtaka kocha Luc kupeleka mawakilishi wake kwenye kesi hiyo, ambapo alijibu kuwa  anatafuta mawakili kutoka Tunisia, ambapo TFF hawana tatizo kwani adhabu zimetolewa baada ya kamati kujiridhisha na kauli hizo kuwa ni zake.