NA ZAINAB ATUPAE
MAKOCHA wa timu za Black Sailors Juma Awadh na KVZ Sheha Khamis, wamezitaka timu zilizoshuka daraja kutoka ligi kuu msimu wa 2019-2020, kutovunjika moyo na kuendelea kupambana.
Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti walisema licha ya kushuka daraja, lakini bado wanao wa muda kupambana na kupata nafasi ya kurudi ligi kuu.
Kocha wa timu ya Black Sailors Juma Awadh amezitaka timu hizo kukubali matokeo na kujiandaa kutafuta njia ambazo zitasaidia kushinda mechi watakazocheza ili kurudi ligi kuu.
Pia alisema wana kazi ngumu kurudi walikotoka,lakini jitihda zao zitawasaidia kutimiza malengo yao wanachotakiwa ni kuwa mashirikiano ya pamoja kati ya viongozi,wachezaji na mashabiki.
Aidha waliwataka viongozi wa timu hizo kushirikiana na mashabiki wao ili kurejesha hamasa ambayo ilipotea baada ya kushuka daraja timu zao.
Alisema timu yake ilishuka daraja lakini alipambana kwa mara ya kwanza na kukosa nafasi,lakini msimu huu ana matumaini makubwa ya kurudi ligi kuu.
Sheha Khamis kocha mkuu wa KVZ alisema timu zote ziko vizuri zinatakiwa kufanya marekebisho madogo madogo ya makosa walioyafanya.
Timu ambazo zimeshuka daraja msimu huu ni pamoja na Jang’ombe Boys ya Unguja, Jamhuri, Machomane, Mwenge, Selem View na Chipukizi zote za Pemba.