BAMAKO, Mali
WINGA wa Wolves, Adamu Traore, ameitwa kwenye kikosi cha Hispania kwa ajili ya mechi za Ligi ya Mataifa ya Ulaya mnamo Septemba dhidi ya Ujerumani na Ukraine.


Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 hajacheza mechi yoyote na taifa hilo, alisema mnamo Januari kwamba bado hajachagua kuichezea Hispania au Mali katika kiwango cha kimataifa.
Aliitwa na Hispania mnamo Novemba, lakini ilibidi ajiondoe kufuatia kupata maumivu.


Winga yoso wa Barcelona, Ansu Fati na wenzake wa Manchester City, Eric Garcia na Ferran Torres pia wameitwa.
Anssumane “Ansu” Fati Vieira ni mwenye asili ya Guinea-Bissau, lakini, anaiwakilisha Hispania kimataifa.


Mechi hizo, ugenini na Ujerumani na nyumbani dhidi ya Ukraine mnamo Septemba 3 na 6 mfululizo, itakuwa ya kwanza kwa Hispania tangu ushindi wa 5-0 dhidi ya Romania mnamo Novemba.


Kikosi kamili kinaundwa na David de Gea (Manchester United), Kepa Arrizabalaga (Chelsea), Unai Simon (Athletic Bilbao), Jesus Navas (Sevilla), Dani Carvajal (Real Madrid), Sergio Ramos (Real Madrid), Pau Torres (Villarreal) na Diego Llorente (Real Sociedad).


Wengine Jose Gaya (Valencia), Sergio Reguilon (Sevilla), Eric Garcia (Manchester City), Fabian Ruiz (Napoli), Thiago Alcantara (Bayern Munich), Sergio Busquets (Barcelona), Rodri (Manchester City), Mikel Merino (Real Sociedad), Dani Olmo (RB Leipzig) na Oscar Rodriguez (Leganes).


Wachezaji wengine ni Rodrigo Moreno (Valencia), Mikel Oyarzabal (Real Sociedad), Adama Traore (Wolves), Marco Asensio (Real Madrid), Ansu Fati (Barcelona), Ferran Torres (Manchester City).(AFP).