WASHINGTON,MAREKANI

RAIS Donald Trump wa Marekani alilazimika kuondolewa ghafla kwenye mkutano na waandishi wa habari katika ikulu ya White House, kufuatia tukio la ufyatuaji risasi nje ya Ikulu hiyo.

Rais Trump aliondolewa dakika tatu tu baada ya kuanza kuzungumza bila ya maelezo yoyote, wakati usalama wa taifa walipomuomba kuondoka.

Muda mfupi baadaye,Trump alirejea na kuwaambia waandishi wa habari kwamba kulikuwa na tukio la ufyatuaji risasi nje ya ikulu.

Alisema, mtu aliyefanya tukio hilo pia alifyatuliwa risasi na vikosi vya usalama na alipelekwa hospitali, ingawa alisema hakujua alikuwa na hali gani.

Hakukua na majeruhi mwengine kwenye tukio hilo,Kulingana na Trump hali ilidhibitiwa.