LONDON, England

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Crystal Palace inayoshiriki Ligi Kuu ya England Wilfred Zaha, amesema anapata wakati mgumu kufungua kurasa za mitandao ya kijamii anazozimiliki, kwa kuhofia maneno ya kibaguzi ambayo hutumwa na watu wanaoendekeza dhambi hiyo.

Mapema mwezi huu kijana wa miaka 12, alishtakiwa kwa kuandika maneno ya kibaguzi kwa mshambuliaji huyo wa Crystal Palace katika mtandao wake wa Instagram (Direct Message).

Zaha anasema ilimbidi pia kujiondoa katika mtandao wa twitter katika simu yake kutokana na kauli za kibaguzi kuzidi kila kukicha.