KAI HAVERTZ
CHELSEA inakaribia kufikia makubaliano ya uhamisho na Bayer Leverkusen kwa mchezaji wa Ujerumani, 21, Kai Havertz. (Teamtalk)
ERIC GARCIA
BARCELONA imemfanya mchezaji wa Manchester City, 19, raia wa Uhispania beki wa kati Eric Garcia kuwa mlengwa wao mkuu kipindi cha usajili kitakapofunguliwa msimu huu. (Goal.com)
AURELIO DE LAURENTIIS
RAIS wa Napoli Aurelio De Laurentiis amesema kwamba beki wa kati wa Senegal Kalidou Koulibaly, anaweza kuruhusiwa kuhama klabu hiyo ikiwa kiwango cha thamani yake cha pauni milioni 81 kitafikiwa. (Sky Italia, via Metro)
OLE GUNNAR SOLSKJAER
KOCHA Ole Gunnar Solskjaer anataka Manchester United kuongeza kasi ya kumsaka mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Uingereza Jadon Sancho, 20, kuepuka hatua ya mvutano iliyojitokeza msimu uliopita kwa Harry Maguire. (ESPN)
MEMPHIS DEPAY
BORUSSIA DORTMUND inaweza kujaribu kumsajili winga wa Uholanzi na aliyekuwa Manchester United Memphis Depay, 26, kutoka Lyon ikiwa United itamsajili Sancho. (Bild – in German)
SERGIO REGUILON
EVERTON imetoa pauni milioni 18 kwa beki wa kushoto raia wa Uhispania wa Real Madrid, 23, Sergio Reguilon. (Sky Sports)
PIERRE-EMERICK AUBAMEYANG
MSHAMBULIAJI wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang alikuwa tayari kuhamia Chelsea Januari lakini Blues ikashindwa kutimiza matakwa ya mchezaji huyo, 31. (Mailonline)
PHILIPPE COUTINHO
KIUNGO wa kati wa Barcelona Philippe Coutinho, 28, amepata ofa ya Arsenal na Tottenham Hotspur, huku kukiwa na uwezekano wa Gunners kumsajili raia huyo wa Brazil na Barca ikipata pauni milioni 9 na kiungo wa kati wa Ufaransa Matteo Guendouzi, 21. (Independent)
MALLIK WILKS
KLABU za Fulham, Bournemouth na Stoke City zote zinamnyatia mshambuliaji wa Uingereza, 21, Mallik Wilks, ambaye ndio amejiunga na Hull City kwa mkataba wa kudumu mwezi uliopita. (Football Insider)