DIEGO CARLOS

WASHINDI wa kombe la FA Arsenal wanamtaka beki wa kati wa Brazil Diego Carlos huku Mikel Arteta, akipanga marekebisho makubwa msimu ujao. (Telegraph – subscription required)

PIERRE-EMERICK AUBAMEYANG

ARSENAL itatoa ofa kwa mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 31, wiki hii ya pauni milioni 250,000 kwa wiki katika makubaliano ya miaka mitatu kuendelea kusalia kwenye klabu hiyo. (Mirror)

DIVOCK ORIGI

ASTON VILLA inamlenga mshambuliaji wa Liverpool, 25, raia wa Ubelgiji Divock Origi. (Sun)

JOSE MOURINHO

KOCHA wa Tottenham Jose Mourinho amepewa fursa ya kumsajili mshambuliaji wa Watford Troy Deeney, 32, kuchukua nafasi ya Harry Kane kwa muda. (Mail)

THIAGO ALCANTARA

LIVERPOOL imeitangulia Paris St-Germain katika kinyang’anyiro cha kutaka kumsajili Thiago Alcantara wa Bayern Munich na sasa hivi ina uwezekano mkubwa wa kumsajili kiungo wa kati wa Uhispania. (Mundo Deportivo, via talkSPORT)

ED WOODWARD

MTENDAJI mkuu wa Manchester United Ed Woodward amefanya mazungumzo na wakala wa mchezaji wa Lille Gabriel Magalhaes juu ya uhamisho wa mlinzi huyo wa Vrazil, 22. (RMC Sport, via Express)

CHRIS SMALLING

MANCHESTER UNITED inamatumaini ya kumtumia mlinzi Chris Smalling, 30, katika makubaliano ya mabadilishano na mlinzi wa Inter Milan, 25, raia wa Slovakia Milan Skriniar – lakini Roma inaendelea na machakato wake wa kumtafuta Mwingereza baada ya kuiridhisha timu hiyo alipokuwa kwa mkopo. (Star)

BEN GODFREY

MABINGWA wa Italia AC Milan na Napoli inafanya mazungumzo na mlinzi wa Uingereza wa timu ya Norwich City, Ben Godfrey, 22, baada ya Canaries kushushwa daraja. (Calciomercato, via Mail)

KIEFFER MOORE

CARDIFF CITY inaongoza kwenye kinyang’anyiro cha kumsaka, 27, wa Barnsley na mshambuliaji wa Wales Kieffer Moore. (WalesOnline)