Ismaila Sarr
KLABU za Liverpool, Crystal Palace na Wolves zimeonesha nia ya kumsajili winga wa Senegal, Ismaila Sarr (22) kutoka Watford iliyoshushwa daraja. (Watford Observer).

Jack Grealish
NAHODHA wa Aston Villa, Jack Grealish (24), atapewa mkataba mpya wa pauni 100,000 wiki moja baada ya Manchester United kuonesha haina nia ya kutaka kumsajili. (Sun).

Sergi Roberto
MANCHESTER City bado haijawasiliana na Barcelona kuhusu beki wa kulia, Sergi Roberto (28), licha ya kuhusishwa kwa kiasi kikuBwa na mchezaji wa kimataifa wa Hispania, na haina mpango huo. (Manchester Evening News).

Aissa Mandi
MABINGWA wa Ligi Kuu ya England, Liverpool inakaribia kumaliza mkataba wa pauni milioni tisa kwa mlinzi wa Real Betis na Algeria, Aissa Mandi (28). (Bein Sports).

Jamal Lewis
LIVERPOOL pia inajitayarisha kwa dau la pauni milioni 10 kwa beki wa kushoto wa Norwich na Ireland Kaskazini, Jamal Lewis (22), wakati inatafuta nani wa kuvaa viatu vya Andy Robertson. (Daily Mirror).

Pierre-Emile Hojbjerg
KIUNGO wa Southampton raia wa Denmark, Pierre-Emile Hojbjerg (24), amepangiwa kujiunga na Tottenham kwa pauni milioni 15, huku beki wa Uingereza, Kyle Walker-Peters (23), akipata mkataba wa kudumu wa pauni milioni 12. (Telegraph).

Francisco Trincao
KLABU ya Leicester City wamefanya mazungumzo na Barcelona kuuliza ikiwa inaweza kumchukua mshambuliaji wa Ureno, Francisco Trincao (20) kwa misimu miwili ya mkopo, ikiwemo wajibu wa kumnunua kwa pauni milioni 45 mwisho wa msimu. (Guardian).

Everton
KLABU ya Everton haitamsajili kiungo, Everton, kwa kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 raia wa Brazil ameonekana kuwa tayari kujiunga na Benfica ya Ureno kutoka Gremio. (Goal).

Deyovaisio Zeefuik
KLABU ya Southampton imeonesha nia ya kumsajili mlinzi wa Groningen, Deyovaisio Zeefuik (22), lakini, Mholanzi huyo anaaminika anapendelea kuhamia Ujerumani. (Southern Daily Echo).

Eberechi Eze
MSHAMBULIAJI wa Queens Park Rangers, Eberechi Eze (22), anamezewa mate na mahasimu wao wa London, Crystal Palace na West Ham, huku klabu hiyo inayoshiriki ligi daraja la kwanza ikiweka thamani ya mchezaji huyo kuwa pauni milioni 20. (Evening Standard).

Angel Gomes
KIUNGO wa zamani wa Manchester United, Angel Gomes (19), amejiunga na klabu ya Ufaransa ya Lille kwa mkataba wa miaka mitano baada ya kuondoka Old Trafford msimu huu. (Metro).

Josh King
KLABU ya Newcastle inammezea mate mshambuliaji wa Bournemouth raia wa Norway, Josh King (28), na kiungo wa kati, David Brooks (23), baada ya ‘Cherries’ kushushwa daraja. (Telegraph).