Pierre -Emerick Aubemayang
MSHAMBULIAJI wa Arsenal na Gabon, Pierre -Emerick Aubemayang (31), anakaribia kutia saini mkataba wa miaka mitatu na klabu hiyo. (Telegraph).

David Silva
KLABU ya Lazio ina imani ya kukamilisha usajili wa kiungo wa kati wa Manchester City, David Silva . Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 atakuwa mchezaji huru mwisho wa msimu huu. (Sky Sports).

Caglar Soyuncu
BARCELONA inajiandaa kuwasilisha dau la pauni milioni 35.9 kwa ajili ya beki wa Leicester mwenye umri wa miaka 24 raia wa Uturuki, Caglar Soyuncu. (NTV Spor).

Jesse Lingard
MANCHESTER United itasikiza ofa za kumuuza kiungo wa kati wa England Jesse Lengard mwenye umri wa miaka 27 . (Guardian)

Declan Rice
WEST Ham haijapokea ombi la kumuuza beki wa kati wa England mwenye umri wa miaka 21, Declan Rice , kulingana na meneja.(Mail).

Callum Wilson
KLABU ya Tottenham itaanza kumuangazia mshambuliaji wa England na Bournemouth mwenye umri wa miaka 28, Callum Wilson. (Express).

Willian
WINGA wa Chelsea na Brazil, Willian (31), amekubali kutia saini mkataba wa miaka mitatu na klabu ya Arsenal utakaogharimu pauni 100,000 kwa wiki. (ESPN).

Diogo Dalot
KLABU ya Everton inamlenga beki wa Manchester United na Ureno, Diogo Dalot (21). (Star).

John Terry
NAIBU meneja wa Aston Villa, John Terry ameorodheshwa katika kuchukua nafasi ya ubosi wa klabu ya Bournemouth ulioko wazi. (Metro).

Nathan Ake
MANCHESTER United walikuwa na azma ya kumsajili beki wa Uholanzi, Nathan Ake (25), kabla ya kujiunga na Manchester City kutoka Bournemouth wiki. (Sky Sports).

Aaron Ramsdale
KLABU ya Bournemouth imekataa ombi la dau la pauni milioni 12 kutoka Sheffield United kumuuza kipa wa England, Aaron Ramsdale mwenye umri wa miaka 22. (Sky Sports).

Ainsley Maitland-Niles
KLABU ya Arsenal imetangaza kwamba iko tayari kumuuza kiungo wa kati wa England, Ainsley Maitland-Niles (22). (Mirror).

Jerome Boateng
BEKI wa Bayern Munich na Ujerumani, Jerome Boateng, amesema, hatosema kwamba hawezi kurudi katika Ligi Kuu ya England. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alihudumu msimu wa 2010-11 akiichezea Manchester City. (Guardian).