BERNARDO SILVA

BARCELONA wanatumai kumshawishi kiungo wa kati Bernardo Silva, 25, aondoke Manchester City na wanaweza kumpatia ofa mchezaji mwenzake wa kimataifa wa Ureno Nelson Semedo, 26, kama sehemu ya mkataba. (Telegraph – subscription required)

DAVID BROOKS

MABINGWA wa Ligi Kuu Liverpool wanapanga kumhamisha kiungo wa kati wa Wales David Brooks, 23, kwa pauni milioni 35 kufuatia kushushwa daraja kwa timu ya Bournemouth. (Sun)

JOSHUA KING

MSHAMBULIAJI wa Bournemouth Joshua King analengwa sana na timu ya Ufaransa Paris St-Germain, huku hasimu wake wa Italia Lazio na Roma wakiwa wanamtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway mwenye umri wa miaka 28. (Sun)

TSIMIKAS

UWEZEKANO wa Tsimikas kuhamia Liverpool ni pigo kwa Leicester, ambao walikua wamempanga kama mchezaji atakayechukua nafasi ya Ben Chilwell, 23, iwapo kiungo huyo wa safu ya nyuma -kulia angeondoka kujiunga na Chelsea msimu huu. (Leicester Mercury)

CHRIS WOOD

MSHAMBULIJI wa Burnley na New Zealand Chris Wood, 28, amepewa ofa ya kujiunga na Lazio. (Corriere dello Sport – in Italian)

ANTONEE ROBINSON

SHEFFIELD UNITED wanamatumaini ya kusaini mkataba na Mmarekani anayecheza safu ya nyuma-kushoto Antonee Robinson fkutoka Wigan kwa pauni milioni 1.5 tu baada ya taarifa ya kushushwa kwa daraja kwa timu ya Latic kuthibitishwa. (Sun)

MESUT OZIL

ARSENAL wako tayari kulipa pauni milioni 18 zilizosalia kwenye mkataba na kiungo wa kati Mjerumani Mesut Ozil ambao unaisha mwaka ujao, au kumpatia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 mshahara wa pauni 350,000- kwa wiki iwapo atahamia katika klabu nyingine (Mirror)

EMILIANO MARTINEZ

KIPA Emiliano Martinez, 27, ameitahadharisha Arsenal kwamba anaweza kuondoka katika timu hiyo, ili kupata muda zaidi wa mchezo ili kuinusuru spot timu ya Argentina . (Continental, via Evening Standard)

YERRY MINA

KIUNGO wa kati-nyuma Mcolombia Yerry Mina, 25, amerudia  utashi wake wa kuhamia Everton huku kukiwa na tetesi juu ya hali yake ya baadae baada ya kubadili mawakala wake . (Liverpool Echo)

ANGEL GOMES

KIUNGO wa zamani wa kati wa Manchester United Angel Gomes, 19, amejiunga na klabu ya Lille lakini Muingereza huyo atacheza kwa mkopo msimu ujao katika klabu ya Ureno ya Boavista. (Guardian)