Gerard Deulofeu
WINGA wa Watford, Gerard Deulofeu, analengwa na Crystal Palace.
Deulofeu anatarajiwa kutafuta uhamisho wa kuondoka Watford, lakini, bado ana mkataba wa kubakia katika barabara ya Vicarage hadi 2023.(Evening Standard).

Tiemoue Bakayoko
KIUNGO wa Chelsea, Tiemoue Bakayoko yuko tayari kupunguza mshahara ajiunge tena na Milan.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye kwa sasa anapata euro milioni sita kwa mwaka alitumia msimu wa 2018-19 kwa mkopo huko San Siro, kabla ya kufunga safari ya muda kwenda Monaco msimu wa joto uliopita.(Calcio Mercato).

Mauricio Pochettino
JUVENTUS wamewasiliana na bosi wa zamani wa Tottenham, Mauricio Pochettino juu ya kupatikana kwake.
Bianconeri wana hamu ya kumleta Muargentina huyo ili achukue nafasi ya Maurizio Sarri, ambaye msimu wa kwanza mjini Turin ametajwa kutofaulu na mashabiki na wataalam kadhaa.(Gazetta dello Sport).

Jorginho
KLABU ya Chelsea imepanga kumuuza, Jorginho kuongeza mfuko kwa ajili ya kiungo wa West Ham, Declan Rice.
‘Blues’ imepanga kuzindua zabuni ya pauni milioni 65 kwa ajili ya Rice, lakini, lazima kwanza iongeze fedha za ziada kutoka kwa mauzo ya wachezaji ili kufadhili mpango huo.(Daily Star).

Willian
NYOTA wa Chelsea, Willian ni ‘mchezaji maalum, kulingana na Paul Merson, anayesisitiza kwamba kiungo huyo ‘atakuwa msainiwa sahihi kwa Arsenal.
Washika bunduki hao wanakaribia kumsaini raia huyo wa Brazil akiwa mchezaji huru akielekea mwisho wa mkataba wake wa sasa na ‘Blues’.(Goal).

Thomas Lemar
KLABU ya Everton ina nia ya kumsaini kiungo wa Atletico Madrid, Thomas Lemar.
‘Toffees’ wanapanga kuzindua ofa rasmi kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ambaye amechukuliwa kuwa ziada kwa mahitaji hapo Wanda Metropolitano.( Le 10 Sport).

Kai Havertz
KLABU ya Chelsea wamepewa onyo la uhamisho katika harakati zao za kumfuata, Kai Havertz, huku Mkurugenzi wa Michezo wa Bayer Leverkusen, Rudi Voller, akisisitiza kwamba ‘Blues’ lazima ifikie masharti yao ili kunasa saini yake.
Kulingana na Goal, Chelsea walifungua mazungumzo na Leverkusen juu ya uwezekano wa euro milioni 76 kwa Havertz, ambaye alikuwa mmoja wa wachezaji walioweka nguvu kwenye Bundesliga mnamo 2019-20.(Goal).

Lucas Torreira
KLABU ya Milan wamembainisha kiungo wa Arsenal, Lucas Torreira, kama mlengwa wa uhamisho.
Rossoneri wanaweza kumnasa raia huyo wa Uruguay ikiwa wataamua kuzindua ofa rasmi, na washika bunduki wapo wazi kwa mauzo katika dirisha la majira ya joto.(Goal).

Alex Meret
KLABU ya Manchester United inamfukuzia mlinda mlango wa Napoli, Alex Meret.
Matarajio ya mlinda mlango nambari moja, David de Gea na Dean Henderson anayecheza kwa mkopo Sheffield United yupo angani.(The Sun).

Harry Wilson
KLABU ya Southampton ipo tayari kuzindua zabuni kwa ajili ya winga wa Liverpool, Harry Wilson.
‘Watakatifu’ hao wanapanga kumnasa nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 kabla ya msimu mpya, lakini, wanaweza kutana na ushindani kutoka Leeds United iliyopanda Ligi Kuu ya England.(Football Insider).