Ben Chilwell
MANCHESTER United wapo tayari kupambana na Chelsea katika soko la uhamisho kwa ajili ya la Ben Chilwell wa Leicester.
‘Blues’ inahusishwa na beki huyo wa kushoto wa England mwenye thamani ya pauni milioni 60 kwa miezi michache iliyopita, na Frank Lampard alikuwa na azma ya kuimarisha safu yake ya kujilinda huko Stamford Bridge.(The Sun).

Dani Ceballos
ARSENAL watakabiliwa na ushindani kutoka kwa angalau klabu tatu kwa ofa ya kumsaini, Dani Ceballos kwenye mkataba wa kudumu.
Milan, Valencia na Real Betis pia wanapendezwa na kiungo huyo Hispania, ambaye ametumia kampeni ya 2019-20 kwa mkopo Emirates akitokea Real Madrid. (The Express).

Adama Traore
JUVENTUS wanataka kumsaini winga wa Wolves, Adama Traore na wapo tayari kutoa wachezaji watatu kama malipo.
Klabu hiyo ya ‘Serie A’ imemuweka Mattia Perin, Daniel Rugani na Cristian Romero mezani kama mpango wa kubadilishana kwa mshambuliaji huyo wa Hispania mwenye umri wa miaka 24.(Sports Mole).

Aaron Ramsey
KIUNGO, Aaron Ramsey hajamridhisha kocha wa Juventus, Andrea Pirlo. Kiungo huyo wa kimataifa wa Wales mwenye umri wa miaka 29 yuko huru kuhamia klabu nyengine. (Mirror).

Jadon Sancho
MANCHESTER United wanaendelea na juhudi za kumsaka winga wa kimataifa wa England, Jadon Sancho, licha ya Borussia Dortmund kusisitiza kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 20 atabakia katika klabu hiyo msimu ujao. (Mail).

Nicolas Otamendi
MANCHESTER City watapokea ada ya pauni milioni nane kumuachilia mlinzi wa Argentina, Nicolas Otamendi (32), msimu huu wa joto. (Sun).

Francisco Trincao
KLABU ya Leicester City inamfuatilia winga wa Barcelona na Ureno, Francisco Trincao (20). (Fabrizio Romano).

Emiliano Buendia
KLABU za Aston Villa na Crystal Palace zinahusishwa na uhamisho wa kiungo mahiri wa Norwich, Muargentina Emiliano Buendia (23). (HITC).

Thiago Alcantara
LIVERPOOL hawatafuta kumsaini beki wa kati wa Bayern, Thiago Alcantara na wekundu hao wanaangalia tu kufanya saini mpya ikiwa ataondoka yoyote muhimu.
Liverpool itaangalia tu kupata fedha yoyote ambayo inakuja kwa wachezaji, lakini, ina uhakika wa kubakisha kikosi chao kilichoshinda taji pamoja.(ESPN).

Papiss Cisse
PAPISS Cisse yuko katika njia ya kuondoka Alanyaspor kwa ajaili wapinzani wao Super Lig ya Uturuki baada ya wakala wake, Sedat Atmaca kuthibitisha mazungumzo mazuri na Besiktas.
Cisse anajiandaa kuondoka uwanja wa Bahsesehir Okullari akiwa mchezaji huru wakati mkataba wake wa miaka miwili utakapomalizika mwishoni mwa msimu wa 2019-20.(Goal).