LIONEL MESSI
MANCHESTER CITY wanaamini wapo nafasi nzuri ya kumsajili Lionel Messi na kuungana na meneja wake wa zamani Pep Guardiola ikiwa mchezaji huyo miaka 33 kutoka Argentina ataondoka Barcelona. (Sunday Mirror)

MAURICIO POCHETTINO
MENEJA wa zamani wa Tottenham Mauricio Pochettino ananafsi kubwa ya kuwa meneja wa Barcelona , wakati klabu hiyo ikiwa na mpango wa kumufukuza Quique Setien siku zijazo. (Guardian)

BEN FOSTER
KIPA wa Watford 37 na ambaye ni kipa wa zamani England Ben Foster anaelekea kwenye usajili mpya ambapo Chelsea na Everton zote zinamuwania. (Sun on Sunday)

BEN CHILWELL
CHELSEA imemaliza mpango wa muda mrefu kumsajili beki wa kushoto wa England Ben Chilwell, 23, kutoka Leicester, ambaye amewagharimu apuni milioni 80. (Independent)
SERGIO RICO
LEICESTER inamuwania kipa wa Sevilla Sergio Rico. Mchezaji huo 26 anacheza kwa mkopo Paris St-Germain. (Sunday Mirror)

MAXWEL CORNET
BORUSSIA inamnyatia mshambuliaji wa Lyon Maxwel Cornet, ambaye alifunga goli la kwanza Jumamosi ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City,lakini mchezaji huyo pia anatakiwa na Wolfsburg. (Le 10 Sport, in French)

JEFF HENDRICK
KIUNGO Jeff Hendrick anajipanga kusaini Newcastle United akiwa huru. Mchezaji huyo 28 kutoka Jamhuri ya Ireland anaondoka Burnley baada ya mkataba wake kufikia tamati Juni 30. (Talksport)

ROB DICKIE
NEWCASTLE pia inavutiwa na beki wa Oxford United na nahodha Rob Dickie, 24. (Sun on Sunday)

CHRIS SMALLING
LICHA ya beki wa Manchester United Chris Smalling, 30, kuendelea kuwepo kwa mkopo Roma, hajapendezewa kuhamia Newcastle. (Mail on Sunday)

THIAGO ALCANTARA
THIAGO ALCANTARA tayari ametoa mkono wa kwa heri kwa Bayern Munich na kiungo huyo miaka 29 kutoka Hispania macho yake ameelekeza kuhamia Liverpool msimu huu. (Talksport)