ANTOINE GRIEZMANN

BARCELONA itasikiliza ofa za mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann, 29, mwaka mmoja tu baada ya kuwasili kutoka Atletico Madrid kwa pauni milioni 107. (Sport via Express)

LIONEL MESSI

LIONEL MESSI ameiambia Barcelona anataka kuondoka klabu hiyo mara moja huku Manchester City ikiongoza katika kinyang’anyiro cha kumwania mshambuliaji huyo, 33, wa Argentina. (Esporte Interativo, via Mirror)

THIAGO ALCANTARA

MCHEZAJI wa Bayern Munich Thiago Alcantara amekubalia mkataba wa miaka minne na Liverpool, huku klabu ya Bundesliga ikitaka ziada ya pauni milioni 30 kwa kiungo huyo wa kati, 29, raia wa Uhispania. (RMC Sport, via Mirror)

PIERRE-EMERICK AUBAMEYANG

ARSENAL imefikia makubaliano na nahodha Pierre-Emerick Aubameyang, 31, juu ya mkataba mpya na pia inafuatilia kwa karibu kumsaini mlinzi wa Brazil Gabriel Magalhaes, 22, kutoka Lille. (Telegraph)

ALEXANDRE LACAZETTE

MABINGWA wa Serie A wanawafuatilia kwa karibu kutaka kuwasajili mshambuliaji wa Arsenal raia wa Ufaransa Alexandre Lacazette au mshambuliaji wa Wolves raia wa Mexico Raul Jimenez, ambao wote wana umri wa miaka 29. (Sky Sports)

PAULO DYBALA

JUVENTUS iko tayari kumuuza Paulo Dybala,26, na Manchester United – na Tottenham zimeonesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji huyo wa Argentina. (Gazetta Dello Sport – in Italian)

TIMOTHY CASTAGNE

LEICESTER inakabiliana na ushindani kutoka kwa Paris St-Germain katika kumwania beki wa Atalanta na Ubelgiji Timothy Castagne, 24. (Calciomercato via Leicestershire Mercury)

CHRIS SMALLING

INTER MILAN inamnyatia mlinzi wa Manchester United Chris Smalling, 30, na huenda ikalipa kitita cha pauni milioni 20 kwa ajili ya mchezaji huyo aliyekuwa beki wa kati wa England. (Metro)

ROBIN KOCH

MACHO ya Leeds United sasa yapo kwa mlinzi wa Ujerumani na Freiburg Robin Koch, 24, huku matumaini ya kufikia makubaliano na ambaye alikuwa mlengwa wao mkuu, beki wa kati wa Brighton Ben White, 22, yakionekana kudidimia. (Telegraph – subscription required)