Kalidou Koulibaly
MANCHESTER City imefufua tena azma yake ya kutaka kumsajili mlinzi wa Napoli raia wa Senegal, Kalidou Koulibaly (29), baada ya kubanduliwa kwenye Ligi ya Mabigwa Ulaya. (La Repubblica).
Jadon Sancho
MKURUGENZI Mtendaji wa Borussia Dortmund, Hans-Joachim Watzke, anadai klabu hiyo haiko chini ya shinikizo lolote la kumuuza mlengwa wa Manchester United, Jadon Sancho (20), licha ya mahesabu kuonesha hasara ya pauni milioni 39.8 kwa kipindi cha mwaka hadi 30 Juni 2020. (Manchester Evening News).
Pierre-Emerick Aubameyang
Arsenal imeanzisha mchakato rasmi wa mkataba mpya wa miaka mitatu wa mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang wenye thamani wa zaidi ya pauni 250,000 kwa wiki. (Mail).
Douglas Costa
MANCHESTER United inamfuatilia kwa karibu winga wa Brazil na Juventus, Douglas Costa (29), inapoanza safari yake ya usajili wa msimu. (Sky Sports).
Edinson Cavani
KLABU ya Benfica ya Ureno inaonekana kuiongoza Leeds United katika kinyang’anyiro cha kumsajili nyota wa Paris St-Germain raia wa Uruguay, Edinson Cavani (30), huku mchezaji huyo, akiwa anapatikana kwa uhamisho wa bure. (Goal).
Junior Caicara
WEST Brom na West Ham wamearifiwa kwamba kitita cha karibu pauni milioni 2.7 kitahitajika kumsajili beki wa Istanbul Basaksehir na Brazil, Junior Caicara (31). (Sport Witness).
Darwin Nunez
KLABU za Brighton na Sheffield United ni miongoni mwa vigogo vinavyomfukuzia mshambuliaji wa Almeria na Uruguay, Darwin Nunez (12) huku mchezaji huyoakitaka malipo ya karibu pauni milioni 14. (Talksport).
Ethan Ampadu
YOSO wa Chelsea, Ethan Ampadu ambaye msimu uliopita alikuwa RB Leipzig kwa mkopo, anajitahidi kumridhisha kocha, Frank Lampard. (Goal).
Abdoulaye Doucourek
KLABU ya Everton imemuulizia kiungo wa Watford, Abdoulaye Doucoure (27). Mchezaji huyo alishuhudia pendekezo la hatua ya kuhamishwa hadi Goodison Park kwa kitita cha pauni milioni 30 ikifeli mwaka mmoja uliopita na sasa yuko huru kuondoka Vicarage Road msimu huu. (Mail).
Kai Havertz
CHELSEA imearifiwa kwamba inahitajika kulipa pauni milioni 90 au ikabiliwe na tishio la kumkosa mchezaji wa Bayer Leverkusen Kai Havertz. (Standard).
Arsene Wenger
KOCHA wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger ameanza kutoa huduma zake kwa Chama cha Soka Uholanzi (KNVB) na kuchukua nafasi ya Ronald Koeman anayetarajia kujiunga na Barcelona. (Mirror).