Rhian Brewster
KLABU ya Tottenham inataka kumchukua mshambuliaji wa Liverpool, Rhian Brewster (21) kwa mkopo. (Football Insider).
Gareth Bale
kocha, Jose Mourinho anataka kumrejesha Tottenham mshambuliaji wa Real Madrid na Wales, Gareth Bale (31). (Cuatro).
Thiago Silva
BEKI wa kati wa Paris St -Germain, Thiago Silva (35), ambaye anaondoka kwenye klabu hiyo ya Ufaransa baada ya fainali za michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya amepewa ofa na Chelsea. (Telegraph).
Jadon Sancho
KUSHINDWA kufikiwa kwa maelewano binafsi ya mkataba wa Muingereza, Jadon Sancho (20), kumeongeza ugumu wa uhamisho wake kutoka Borussia Dortmund kwenda Manchester United. (ESPN).
Sergio Romero
MANCHESTER United wanaweza kuipatia Aston Villa mlinda mlango, Sergio Romero (33), kama sehemu ya makubaliano ili kumpata kiungo, Jack Grealish (24). (Mail).
Federico Bernardeschi
KLABU za Chelsea na Atletico Madrid zina mpango wa kumpata winga, Federico Bernardeschi (26), anayekipiga Juventus. ( Calciomercato).
Harry Wilson
KLABU ya Liverpool inajiandaa kumuuza kiungo, Marko Grujic (24), na winga, Harry Wilson (23), msimu huu. (Mirror).
Kai Havertz
CHELSEA watakamilisha kumsajili kiungo wa Ujerumani, Kai Havertz (21), wiki hii kwa mkataba wa miaka mitano iwapo wao na Bayer Leverkusen wanaweza kupunguza tofauti ya pauni milioni 18 ya thamani ya mchezaji huyo. (Telegraph).
Andreas Pereira
KIUNGO wa Manchester United raia wa Brazil, Andreas Pereira (24), analengwa na Benfica na Valencia. (ESPN).
Alex Sandro
MANCHESTER United imerejesha azma yao kwa beki wa kushoto, Alex Sandro (29), anayeichezea Juventus. ( Calciomercato).
Ben White
KLABU ya Leeds imetoa ofa ya tatu inayoaminika kuwa takribani pauni milioni 25 kwa ajili ya mchezaji wa nafasi ya ulinzi, Ben White (22). (Sky Sports).
Adama Traore
KLABU ya Wolves ipo tayari kusikiliza ofa kubwa kwa ajili ya winga, Adama Traore, ingawa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, bado amesaliwa na miaka mitatu ya kuutumikia mkataba wake. (Mail).