ZASPOTI
Benjamin Pavard
KLABU ya Paris Saint-Germain wanatafuta saini ya mlinzi wa Bayern Munich, Benjamin Pavard.
FCB wameripoti kuweka bei ya kuuliza ya karibu pauni milioni 45 kwa mshindi huyo wa Kombe la Dunia, ambaye anaweza kucheza kulia au beki wa kati.( L’Equipe).
Eric Garcia
BARCELONA wametoa ofa ya euro milioni 10 kwa yoso wa Manchester City, Eric Garcia.
Miamba hiyo ya Katalunya inangojea jibu la ManCity, lakini, hawako tayari kuongeza ada hiyo. Ikiwa ManCity itakataa ofa hiyo, Barca itangojea hadi Januari ili impate kwa bei ya chini au umsaini bure msimu wa joto ujao.(Mundo Deportivo ).
Ben Chilwell
KLABU za Chelsea na Leicester zinakaribia makubaliano kwa ajili ya beki wa kushoto, Ben Chilwell.
Nyota huyo wa Leicester amekuwa juu kwenye orodha ya ununuzi wa ‘Blues’ kwa muda mrefu na ana hamu ya kubadili kwenda Stamford Bridge.(Sky Sports).
Eduardo Camavinga
KIUNGO, Eduardo Camavinga, amesisitiza atabakia Rennes kwa msimu wa 2020-21 huku kukiwa na uvumi wa kuhamia Real Madrid.
Nyota huyo amekuwa na msimu bora akiwa na miamba hiyo.(Goal).
Alessandro Florenzi
BEKI, Alessandro Florenzi anawaniwa na Everton na Atalanta huku Inter ikiwa ndiyo klabu ya karibuni kutaka kumsajili.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 alitumia sehemu ya msimu uliopita kwa mkopo huko Valencia kutoka Roma na anatarajiwa kuendelea tena msimu huu wa joto.(CalcioMercato.com).
Serge Aurier
AC Milan waPo tayari kulenga uhamisho kwa ajili ya kiungo wa Tottenham, Serge Aurier.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Ivory Coast amejitahidi kushinda dhidi ya Jose Mourinho, lakini, hakuna mpango wowote ambao umekubalika kati ya klabu hzio.(Gazzetta dello Sport)
Alexandre Pato
KIUNGO, Alexandre Pato, ametangaza kwamba ataondoka Sao Paulo.
Nyota huyo amekuwa na kiwango bora katika msimu huu unaoelekea mwishoni.(Goal).
Robin Koch
KLABU ya Leeda ipo tayari kwa uhamisho kwa ajili ya mlinzi wa Freiburg, Robin Koch.
Beki huyo wa kati mwenye thamani ya pauni milioni 20 pia anatakiwa na Tottenham. (The Sun).
Antonio Conte
KOCHA Mkuu wa Inter, Antonio Conte, alisema kwamba huenda hatokuwepo San Siro.
Mtaliano huyo alishuhudia kikosi chake kilitandikwa magoli 3-2 na Sevilla, akimaliza kampeni ambayo imeonekana kukosana na uongozi wa Inter.(Goal).
Isak Hansen-Aaroen
KLABU ya Tromso ya Norway imethibitisha, Isak Hansen-Aaroen, anaondoka baada ya kukubaliana kusaini na Manchester United.
Mshambuliaji huyo aliyeanza soka ya wakubwa na Tromso akiwa na umri wa miaka 15 anafikiriwa kuwa nyota hapo baadaye.(Goal).