ODSONNE EDOUARD
ASTON VILLA itatangaza dau la pauni milioni 30 la kumnunua mshambuliaji wa Celtic Mfaransa Odsonne Edouard, 22. (The Scottish Sun)
GABRIEL MAGALHAES

KIUNGO wa safu ya kati-nyuma wa Lille raia wa Brazil Gabriel Magalhaes, 22, amekubali kujiunga na Arsenal na atakamilisha uhamisho wake wa pauini milioni 27 wiki ijayo. (The Guardian)
DAVID BROOKS

BOURNEMOUTH haitawazuia wachezaji wanaotaka kuhama – hatua ambayo imeifungulia mlango Manchester United kumsajili winga wa Wales David Brooks, 23. (Daily Mail)
RONALD KOEMAN

MKUFUNZI mpya wa Barcelona Ronald Koeman anataka kuwasajili mshambuliaji wa Inter Milan Muargentina Lautaro Martinez, 23, mlinzi wa safu ya kati na nyuma wa Manchester City Mhispania Eric Garcia, 19, na beki wa Valencia Mhispania Jose Gaya, 19. (Sport – in Spanish)
NICOLAS TAGLIAFICO

KLABU hiyo ya Catalan pia inamtaka kiungo wa safu ya kati ya nyuma wa Ajax Muargentina Nicolas Tagliafico, 27. (Marca)
DIMITRIS GIANNOULIS

NEWCASTLE wametoa ofa ya pauni milioni 4.5 kwa klabu ya Ugiriki ya PAOK kumnunua mchezaji wa beki Dimitris Giannoulis,24. (Manu Lonjon via Sports Lens)
ANDREAS GEORGSON

KOCHA wa Arsenal Mikel Arteta anapania kumvuta kocha wa Brentford na mtaalamu Andreas Georgson kuwa sehemu ya kikosi cha ufundi. (London Standard)
ISAK HANSEN-AAROEN

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Tromso raia wa Norway Isak Hansen-Aaroen, 16, amethibitisha katika mitandao ya kijamii kuwa atahamia Manchester United. (Mirror)
LIONEL MESSI

LUIS FIGO hatarajii mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 33, akifuata nyayo zake kwa kuondoka Barcelona na kuhamia Real Madrid. (Marca)
ZLATAN IBRAHIMOVIC

MSHAMBULIAJI wa Uswidi Zlatan Ibrahimovic, 38, bado hajasaini mkataba mpya AC Milan. Mchezaji nguli huyo atasalia bila timu mkataba wake utakapo kamilika mwisho wa mwezi Agost. (Gazzetta dello Sport – in Italian)