Luis Suarez
BARCELONA itakatiza kandarasi ya mshambuliaji wa Uruguay mwenye umri wa miaka 33, Luis Suarez. (RAC1).

Nicolas Gonzalez
LEEDS United wanamtaka mshambuliaji wa Argentina, Nicolas Gonzalez (22), amesema, mkurugenzi wa michezo wa Stuttgart, Sven Mislintat. (Yorkshire Evening Post).

Allan
KLABU ya Everton wameafikia mkataba na Napoli kulipa pauni milioni 31.5 ili kumpata kiungo wao wa kati, Mbrazil Allan (29). (Daily Express).

Moise Kean
MSHAMBULIAJI wa Italia, Moise Kean (20), anakaribia kukamilisha mchakato wa kurudi katika klabu yake ya zamani ya Juventus kwa mkopo. (Tuttosport).

Victor Lindelof
MLINZI wa Manchester United, Victor Lindelof (26), amepongezwa na polisi wa Uswisi kwa kumkamata mwizi aliyekuwa amemuibia ‘ajuza’. (Sky Sports).

Ainsley Maitland-Niles
KLABU ya Wolves wamepiga hatua katika mazungumzo yao na Arsenal kuhusu mkataba wa miaka minne wa beki Muingereza, Ainsley Maitland-Niles (22). (Sky Sports).

Joel Pereira
MANCHESTER United wapo tayari kumpeleka kwa mkopo kipa wao Moreno, Joel Pereira (24), kwa Huddersfield. (The Sun).

Borja Mayoral
KLABU ya Valencia wanamfuatilia kwa karibu mshambuliaji wa Real Madrid, Muhispania Borja Mayoral (23). (Mundo Deportivo).