Rhian Brewster
KLABU ya Newcastle imeungana na klabu nyengine za ligi kuu zinazomuania mshambuliaji wa Liverpool, Rhian Brewster (20). (Chronicle).

Pep Guardiola
MSHAMBULIAJI wa Argentina, Lionel Messi, amewasiliana na meneja wa Manchester City, Pep Guardiola na kumfahamisha kwamba anataka kuondoka Barcelona. (Times).

Eric Garcia
MANCHESTER City inaweza kuwatoa mabeki wake raia wa Hispania, Eric Garcia (19), na Angelino (23), kama chambo ili kumnasa Messi, kama hawatamsainisha akiwa mchezaji huru.(Mail).

Gabriel Jesus
MANCHESTER City inajiandaa kuipa Barcelona kitita cha pauni milioni 89.5 pamoja na Garcia, kiungo wa Ureno Bernardo Silva (26), na mshambuliji wa Brazil, Gabriel Jesus (23), kwa ajili ya kumnasa Messi. (Sport).

Sergio Reguilon
REAL Madrid inataka euro milioni 20 kwa ajili ya beki wake wa kushoto wa Hispania, Sergio Reguilon (23) ambaye alizivutia klabu za Manchester United, Tottenham, Juventus na Inter Milan wakati akicheza kwa mkopo Sevilla. (Marca).

Matt Doherty
KUWASILI kwa beki wa kulia raia wa Ireland, Matt Doherty (28), Tottenham kutoka Wolves kunaweza kuwa tiketi ya mlinzi wa Ivory Coast, Serge Aurier (27), kuondoka. (Standard).

Serge Aurier
TOTTENHAM imekataa ofa ya kwanza kutoka AC Milan kwa ajili ya Serge Aurier, huku Bayer Leverkusen ikionyesha nia ya kutaka huduma ya mlinzi huyo. (Sky Sports).

Sandro Tonali
MANCHESTER United imewasilisha ombi la kumnasa kiungo wa Brescia, Sandro Tonali (20), ambaye anatajwa kama mmoja wa makinda wanaokuja juu nchini Italia. (Corriere dello Sport).

Luiz Felipe
KLABU ya Leeds inajiandaa kupeleka ombi la kumnasa beki wa kati wa Brazil anayekipiga Lazio, Luiz Felipe (23). (Talksport).

Kristoffer Ajer
WAWAKILISHI wa mlinzi wa Norway, Kristoffer Ajer (22), na kiungo wa Ufaransa, Olivier Ntcham (24), wameitaka klabu ya Celtic kutaja thamani za wachezaji hao kabla ya kutimka. (Sky Sports).

Troy Deeney
NAHODHA na mshambuliaji wa Watford, Troy Deeney (32), amewekwa sokoni kwa West Brom. (Mail).