LIONEL MESSI
MAAFISA wakuu katika klabu ya Barcelona wanatarajia kwamba kiungo mchezeshaji wa Argentina Lionel Messi ,33 atajiungana na Manchester City. (Telegraph – subscription required)

JAMES RODRIGUEZ
MCHEZAJI wa Colombia James Rodriguez, 29, atafanyiwa vipimo vya kimatibabu katika klabu ya Everton wiki ijayo, klabu hiyo ikikaribia kuafikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji huyo wa Real Madrid. (Talksport)

SERGE AURIER
BEKI wa Tottenham na Ivory Coast Serge Aurier, 27, amekataa uhamisho wa kuelekea Wolves baada ya kujumuishwa katika mpango wa uhamisho wa mchezaji wa Ireland Matt Doherty 28 kujiunga na Tottenham. (Star)

TANGUY NDOMBELE
INTER MILAN wameambia Tottenham wana hamu ya kumsaini Tanguy Ndombele lakini wanaitaka klabu hiyo kupunguza thamani ya pauni milioni 55 ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 raia wa. (Express)

DONNY VAN DE BEEK
KIUNGO wa kati wa Ajax na Uholanzi Donny van de Beek, 23,anasubiri kuona iwapo Barcelona itawawasilisha ombi la kutaka kumnunua kabla ya kufikiria uhamisho wa Manchester United au Tottenham. (Sport)

KEVIN DE BRUYNE
MPANGO wa Manchester City kutaka kumpatia kandarasi mpya ya pauni 350,000 kwa wiki kiungo wake wa kati Kevin De Bruyne umezuiliwa kufuatiwa kukamatwa kwa ajenti wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 (Mirror)

ROB HOLDING
NEWCASTLE imejitokeza kama timu itakayomsajili beki wa Arsenal na England Rob Holding, 24, kwa mkopo wa muda mrefu. (The Athletic – subscription required)

AINSLEY MAITLAND-NILES
NEWCASTLE imemuulizia beki wa Arsenal Ainsley Maitland-Niles, 23, lakini wamevunjwa moyo na bei ya pauni milioni 25 inayotolewa na Arsenal. The Gunners walikataa ombi la pauni milioni 15 kutoka kwa Wolves wiki iliopita . (Telegraph – subscription required)

EMI MARTINEZ
ASTON VILLA inandaa ofa ya pauni milioni 10 kumnunua kipa wa Arsenal raia wa Argentina Emi Martinez, 27. (Independent)