ZURICH, Uswis
RAIS wa Shirikisho la Kandanda Ulaya (UEFA) Aleksander Ceferin atafanya mazungumzo juu ya kuendelea na mfumo wa mtoano wa mkondo mmoja, ambao umetumika kukamilisha msimu wa ligi ya mabingwa na Europa msimu huu.
Mfumo huo umetumika ili kuokoa msimu huu uliovurugika kutokana na janga la virusi vya corona, hata hivyo unaweza kutumika tu katika awamu ya nusu fainali.
Katika mahojiano na shirika la habari la ‘Associated Press’ siku ya Jumapili, Ceferin alisema watu ndani ya masuala ya kandanda na nje wamewasiliana nae na kusema walikuwa “wamefurahishwa mno”
Kutokana na mfumo wa timu nane katika fainali ambao umeachana na mfumo wa michezo miwili ya nyumbani na ugenini katika robo fainali na nusu fainali.
“Naweza kusema kuwa mfumo huu wa mchezo wa mkondo mmoja unaonekana kuleta hamasa zaidi kuliko mfumo mwingine wa michezo miwili,” Ceferin aliliambia shirika la habari la AP kabla ya Paris Saint-Germain kucheza dhidi ya Bayern Munich katika fainali ya ligi ya mabingwa.
“Ni moja kati ya mambo yenye kutia msisimko ambayo yamesababishwa na janga hili,” Ceferin alisema.